

Mkutano wa eLearning Africa kwa mwaka 2011 unampango wa kuwaweka na kuwakutanisha pamoja zaidi ya watoa mada 260 kutoa nchi 49 tofauti. Wanatarajiwa kuwa na watoa mada na wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa yakiwemo UNEP, UNESCO/UNEVOC, Banki ya Dunia pamoja na taasisi mbalimbali za elimu zilizopo Afrika kwa ujumla.
Berlin, Germany. Dar es Salaam, Tanzania. Kwa Mwaka huu wa 2011 eLearning Africa itahakikisha inawawezesha vijana wa Afrika kutambua umuhimu wao na kutumia kikamilifu na kwa ubunifu nyenzo ya elimu zinazo patikana kwa wote na bure kwa njia ya teknolojia ambayo inajulikana kama Open Educational Resources (OERs). Pia mafunzo ya kutoa taaluma kwa kupitia mtandao wa kumpyuta pamoja na technohama katika kuelimishana masuala muhimu ya Afya ya jamii, kilimo bora pamoja na taaluma za kibenki barani Afrika itatolewa.
Dondoo na Agenda za mkutano huu muhimu kwa sasa unaweza kuperuzi na kuzipata kwenye tovuti http://tinyurl.com/4x82o48
Mkutano huu mkubwa wa eLearning Africa utahusisha nchi zote za Pan-Afrika na unalenga zaidi kuendeleza sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICTs) kwa kutoa elimu na mafunzo. Mkutano huu utafanyika Dar es Salaam TANZANIA kuanzia mei 25 hadi 27.
Kutakuwa na vipengele 6 vitakavyokuwa vinaongelea ‘Ujana, ujuzi na jinsi kijana anavyoweza kujiajiri mwenyewe. Kipengele cha ‘Wazup? Youth Voices on Life, Love and eLearning’ kitakagusia maswala ya maisha, mapenzi na elimu kwa kupitia teknolojia ya vijana, itakuwa ikiendelezwa na kukamilishwa na vijana wenyewe. Watabadilishana mawazo wao wenyewe ili kufahamu maana ya kuwa kijana wa kisasa au digital katika jamii wanazoishi pamoja na uhusiano walionao na kizazi kilichopitwa na teknoljia za kisasa.
Pia kutakuwa na vipengele 10 vitakavyoongelea mada mbalimbali kama Kijana na Ujasiliamali, Uelewa wa takwimu, jinsi ya kutumia sanaa na ubunifu kujiajiri mwenyewe, au jinsi ya kuboresha vijana wenye ulemavu wa kusikia. Mwaka huu mkutano wa TVET utalenga zaidi kuinua vipaji vya vijana na watu wazima wanaotaka kujifunza kupitia mikakati ya kisasa inayotumia teknolojia.
Mafunzo kwa Walimu yatapewa nafasi kubwa sana mwaka huu. Mada zitaongelea kufundisha kwa njia ya video na simu za mkononi nchini Tanzania, pamoja na kuondoa hofu ya waalimu katika kutumia teknolojia mpya. Mazungumzo yatatokana na mafunzo na uzoefu uliopatikana katika bara la Asia (Vietnam, Singapore na Korea ya Kusini)
Mafunzo maalum kwaajili ya sekta za Afya ya jamii, Fedha, na Kilimo yatatolewa. Hii ni pamoja na ‘Jinsi gani ujumbe mfupi kwa njia ya simu (yaani SMS)zinazoweza kuokoa kuboresha maisha nchini Malawi’,’Elimu ya kuendeleza ujuzi na utaalamu kwenye kilimo kwa njia ya vyombo vya habari’ na ‘Teknolojia ya habari na mawasiliano kwenye maswala ya kibenki huko Mozambique.’
Elimu kwa njia ya Simu za mkononi itakuwa mada kali na ya kusisimua, hii ni kutokana na matumizi na uhitaji wake ambao unaonekana kuchukua nafasi kubwa sana katika mazingira ya kila siku pamoja na jamii kuwa na viashiria vya kukua kwa uelewa wake kila siku.
Pia kutakuwa na njia mbadala ya kubadilisha mawazo zijulikanazo kama “Umoja sessions”. Hizi zitakuwa maalum kwa ajili ya kuchangia mawazo na ujuzi wa miradi au mambo mbalimbali.
Nyenzo za Elimu ya bure na kwa wote kwa njia ya teknolojia au Open Educational Resources (OER) imekuwa mada muhimu katika bara la Afrika. Mwaka huu mkutano utaangalia kwa makini matumizi ya elimu kwa njia hii.
Mazungumzo ya eLearning Africa ita dadisi na kujadili yafuatayo:
Mfumo wa Elimu kwa njia hii inakuwa na mapungufu kwasababu ya kuamini vyuo na taasisi za kielimu wakotayari kutoa nyenzo na vifaa bure kwa wote.
Kwa ajili ya kukuza na kuwaendeleza watafiti watokao Afrika wanaofanya utafiti wa elimu kwa njia ya teknolojia, kituo kipya kimeundwa maalum kwa ajili hii. Hii itawezesha utafiti katika bara nzima.
Washiriki watapata nafasi ya kukutana na watafiti hao na kujifunza kutoka kwenye vile walivyovivumbua ikiwa ni pamoja na kujiwekea mitazamo ya kimaendelea kulingana na watakachojifunza pamoja na kuwa na mikakati ya kupambana na changamoto zinazofuatia hapo baadae.
Sasa katika mwaka wake wa sita, eLearning Afrika imekua ikijijenga kama nyenzo maalum inayolenga kukuza sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano au teknohama (ICT) kwa kutoa elimu na mafunzo barani Afrika. Dhamira yake ni kuwakutanisha na kuwawezesha kwa pamoja watu wote wenye fikra endelevu ili waweze kuendeleza waliyoyapata wakiwa shuleni, vyuoni, kwenye mafunzo na walsha maalum au sekta maalum za elimu binafsi walizopitia awali.
taarifa zaidi zinapatikana kwa kubofya www.elearning-africa.com.
eLA kwa kifupi
eLearning Africa, 6th International Conference on ICT for Development, Education and Training
May 25–27, 2011
Mlimani City Conference Centre, Dar es Salaam, Tanzania
Organisers: ICWE GmbH, www.icwe.net, Government of the Republic of Tanzania
Contact: ICWE GmbH, Ms Katharina Goetze,
info@elearning-africa.com, www.eLearning-africa.com
Tel.: +49 (0)30 310 18 18-0
Press Contact
ICWE GmbH
Ms Beate Timmer
Tel.: +49 (0)30 310 18 18-0, press-service@icwe.net
Press releases
www.elearning-africa.com/press_release.php
Photographs
www.elearning-africa.com/media_library_galleries.php
News Portal
www.elearning-africa.com/eLA_Newsportal
www.ela-newsportal.com