

eLearning Africa imejianzisha yenyewe kama mkutano kuu wa Bara wa kila mwaka katika matumizi ya Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano (ICT) kwa ustawi, elimu na mafunzo.
Kuhamia nchi nyingine kila mwaka, tunawaunganisha washikadau, wataalamu na weledi kutoka kwa usuli zote na viwango – kutoka kwa mawaziri kwa watafiti, walimu kwa wanafunzi, watu wa biashara kwa wataalamu wa mfunzo na ustawi, watumishi wa serikali na watoaji teknolojia.
Anuwai tele, warsha zetu, vikao na mazoezi ya ufafanuzi-bora inajumlisha vipengele vyote vya ubora wa mafunzo ya ICT kwa Kiingereza na Kifaransa. Kuchachawisha mijadala, kuharakisha vikao vya kujuana, mikahawa maalum ya manufaa ya mafunzo na mapokezi tofauti zinatoa fursa nyingi za kukuza elimu, kuunda mawasiliano mpya na kufanya biashara.
Tangu kuanzishwa kwa eLearning Africa mwaka wa 2006, hesabu ya washiriki imeongezeka zaidi ya maradufu, kutoka wajumbe 832 katika utangulizi wa tukio, hadi wajumbe 1778 huko Lusaka, Zambia, mwaka wa 2010. Na kati ya asilimia 70 hadi 80 ya washiriki wanaotoka Afrika, mkutano huo ni tukio la kweli la Afrika-yote. Mikutano ya hapo awali ambayo ilifanywa Uhabeshi, Kenya, Ghana, Segegali na Zambia. eLearning Africa ijayo itakuwa Dar es Salaam, Tanzania, kutoka Mei 25 – 27, 2011.
eLearning Africa imekuzwa na kupangwa na ICWE, wataalamu wanaoongoza katika matukio ya kimataifa na miradi ya elimu na mafunzo, ikiungana na wizara za elimu na muundo msingi katika nchi zinazohusika, pamoja na washiriki wa kimataifa na Afrika.
Lengo kuu la eLearning Africa ni kujifunza, kugawana na kujuana, pia kukweza upanuzi katika Nyanja ya uboreshaji wa elimu-ICT Afrika
Tunatamani kukuza jumuiya inayokuwa kuhusu utendaji katika nyanja hii, kugawana rasilimali na kusaidia utafiti maalum wa Afrika. Kuauni jukwaa kichechemo, eLA inalenga kuanzisha uvumbuzi wa dhana, kuanzisha ushirikiano mpya na kusaidia ubia kwa sekta ya umma na binafsi.
Lengo la mwisho la eLearning Africa ni rahisisha na kusaidia kuendeleza ustawi.
Kuna uanzisho nyingi za ICT zinazoendelea Afrika pia katika maeneo mengine ya dunia yanayostawi, na zote zinakumbwa na changamoto kama hizo. Kwa kuleta uanzisho hizi pamoja, eLearning Africa inalenga kubuni kushirikiana kwa vitendo vya ustawi-kibinafsi.
Kwa nchi zinazokaribisha, mikutano inatoa fursa zisizo sawa kukweza upanuzi kuhusu uwezekano wa elimu ya ICT miongoni mwa watoaji uamuzi-kisiasa, weledi wa elimu na watoaji elimu. Mara nyingi mikutano inafikia kilele cha kampeni ya kitaifa kusaidia sera ya nchi katika “ICT kwa elimu“.
eLearning Africa inaoa jukwaa muhimu ya “ajenda ya African-yote” kutosheleza mahitaji na changamoto za utekelezaji wa ICT katika elimu, kuwaleta washika dau wengi pamoja kwa meza moja.
Kuzunguka kote Afrika, tunawaunganisha watoaji-uamuzi kutoka kwa serikali na kiwanda na wataalamu na weledi kutoka kwa vyuo vikuu, shule na watoaji mafunzo, pia na wenzi katika ushirikiano wa ustawi.
eLA inaunga mkono kikamilifu kutafuta ushirikiano wa serikali za Afrika ambazo ziko tayari na zina uwezo wa kusaidia tukio kwa kuwa kama nchi inayokaribisha wageni.
Zaidi ya hayo, tunashirikiana na idadi kubwa ya mawakala za ustawi, mashirika ya kimataifa na taasisi za elimu, zote zinahusika kwa njia moja au nyingine pamoja na Afrika. eLA inajenga thabiti mtandao wake wa kusaidia tukio na kuhakikisha mwendelezo.
eLearning Africa inahimiza kushiriki anuwai. Tunawashirikisha watumishi wenye madaraka rasmi wakubwa wa serikali, pia na wataalamu na weledi kutoka kwa elimu na mafunzo inayoongoza. Hatutamani kuwa mkutano wa kipekee ya wataalamu wa hali ya juu pekee.
Wajumbe wanao wakilisha serikali na wakala za serikali, wachezaji wa ulimwengu katika kiwanda cha elimu, pia na SMEs. Wanatoka kwa shule, vyuo vikuu, taasisi za kisayansi na elimu ya juu, pia kutoka kwa mwungano na mashirika katika nyanja ya ustawi na elimu.
Ingawaje wengi wa washiriki wanaweza kuhudhuria tukio kwa kujitegemea wao wenyewe, eLA inaendelea mikakati yake fanisi ya kushiriki iliyofadhiliwa-wahisani ya wajumbe wa Africa kupitia eLearning Africa Scholarship Trust EAST (www.easttrust.org), kuhakikisha usawazishaji wa usawa kati ya wanachama wa mkutano wa hadhira, kama uwezo wa kifedha ya nchi za Afrika ni anuwai mno.
Tangu 2006, wasomi wa eLearning Africa wamekuwa wakisaidiwa na vyuo na taasisi tofauti kama SPIDER (Mpango wa Kiswidi ya ICT katika Maeneo Yanayostawi), Msingi wa William na Flora Hewlett, Shirika la Carnegie ya New York, African Development Bank, Msingi wa John D. na Catherine T. MacArthur, Msingi wa Andrew W. Mellon, Msingi wa Rockefeller na wengine wengi.
Ufikivu wa taarifa ni muhimu kwa ustawi kokote duniani.
Taarifa ya matibabu ya dawa inaweza kuokoa maisha, elimu kuhusu mbinu mahususi za ukulima inaweza kusaidia kubuni mapato mapya, watafiti wa vyuo vikuu watafaidika na utambuzi mpya ya kisayansi, kama wanaweza kujadili dhana na matokeo na wenzao katika sehemu zingine za dunia.
Teknolojia za Taarifa na Mawasiliano – Mtandao, tarakilishi, vifaa vya mkononi, vipindi vya masomo ya mtandao – inaruhusu ufikivu kwa taarifa. Mengi ni kuwa, ICT inawapa watu fursa nyingi ya mafunzo yasiyo na utaratibu na ya kujifunza-mwenyewe. Wanaweza kujifunza wakati wowote na kokote na katika hali yoyote ya maisha huenda wakawa.
Mafunzo ya wakati-ufaao na kujifunza mwenyewe ina motisha sana, na ICT inaweza kutekelezwa katika kiwango kikubwa. Kwa hivyo, ICT na masomo ya mtandao inaweza kusaidia Afrika na umati wake inayokua kuharakisha ustawi na kubadilisha maisha ya watu wake.
Mifano chache:
Saharan-ndogo ya Afrika, milioni nne zaidi watahitajika kufikia 2015? Tanzania, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Utaalamu, wakishirikiana na kampuni za teknolojia za kimataifa, zinatoa tarakilishi, maudhui ya masomo ya mtandao na mafunzo ya ICT kwa shule na walimu katika juhudi ya kutatua upungufu wa walimu 85,000. Zambia, walimu 30,000 wamejihami na tarakilishi ndogo zenye kutumia nguvu-fanisi, ya kuwaruhusu kupata ujuzi wa ICT na ufikivu wa rasilimali za mafunzo.
Maelfu ya wanafunzi wa shule za upili huko Zambia, Nijeria, Misri, Ghana, Libya na Afrika Kusini wanajifunza hisabati na sayansi kupitia kipindi fanisi na cha kisasa cha eLearning.
Hadi sasa, African Virtual University imetoa shahada kwa wanafunzi 40,000 kote Afrika. Ina maeneo katika zaidi ya nchi thelathini katika Afrika Saharan-ndogo, ni Mtandao kubwa kabisa la bara ya taasisi wazi ya masomo na masomo ya mtandao.
Kufungua na kuanzisha ufikivu inaleta utafiti wa kisasa katika udaktari, kilimo na uhandisi kwa vyuo vikuu vya Afrika kwa kuwapa ufikivu wa bure kwa zaidi ya shajara 5,000 za kitaaluma.
Riwaya ya simu ya mkononi iliyo kwa lugha ya Kiingereza na isiXhosa imewafikia vijana 17,000 wa Afrika Kusini katika ya 2009 na 2010, imeboresha pakubwa ujuzi wao wa kusoma na kuandika.
Elimu ya programu ya simu ya mkono imesaidia biashara ya kilimo kote Barani. Kenya, mahali ambapo kilimo inachangia asilimia 25 ya thamani ya vitu vinavyotolewa kwa soko, wakulima wadogo wanajifunza jinsi ya kuboresha biashara yao kwa kutumia simu za mkono, ilhali wakati huo huo ikihifadhi rasilimali asili na mazingira.
Kibanda kitembeacho cha Mtandao inaleta taarifa, fursa za ujasiriamali, rasilimali za mafunzo na njia za mawasiliano kwa jumuiya za vijijini Afrika.
Tunahimiza majidiliano wazi ya lini na wapi ICT inaweza kutumiwa ipaswavyo na wapi wanatoa manufaa ya kweli ukilinganisha na vifaa vingine vya elimu. Shinikizo letu si tu kwa teknolojia kwa ajili yake.
eLearning Africa 2011 istasherekea maadhimish ya sita ya tukio. Watu wengi wanatuambia kuwa wakati huu wa kipindi cha muda mfupi, mikutano imeleta tofauti kubwa.
Tumesaidia kubuni jumuiya ya Afrika-yote ya mazoezi kwa kuanzisha na kusaidia ushirikiano mpya, mitandao na ubia.
Katika mkutano wa kwanza mwaka wa 2006, majadiliano mengi yalilenga kwa ukweli kwamba Afrika kwa wakati mrefu haikuwa na muunganisho wa kasi na nafuu pamoja na ulimwenguni. Kwa sasa, lengo limebadilika. Sasa majadiliano mengi inahusu maudhui, ufundishaji na makadirio. Kuna tamanio la ‘kupima’ faida za mafunzo ya teknolojia inayotoa, na mada ya kibinafsi imekuwa maalum zaidi na ya kawaida.
Mabadiliko haya ni kwa ajili ya ukweli kwamba muunganisho na ufikivu imekuwa ikiendelea vizuri pole pole, simu za mkono zimeenea kila mahali karibu kwa kila nchi zote za Afrika, na watu sasa ‘wanaelewa tekhnolojia’, Afrika na kote duniani.
Pamoja na kuwepo kwa maarifa mengi kuagawana katika mtandao na mfululizo wa ushirikiano ambao eLearning Africa imeweza kukuanzisha, mkutano wetu imetenda wajibu muhimu katika ustawi huu.
Kuongezea, sisi wenyewe tumefanya taarifa na rasilimali kuwepo. Tangu 2006, kila wakati tumekuwa tukifuatilia matukio ya African eLearning na kuchapisha mamia ya hadithi za marejeo kuhusu vile teknolojia inatumika kwa elimu katika bara la Afrika katika lango la habari za eLearning Africa. Hadithi zinajumlisha sekta zote za elimu inayofadhiliwa-teknolojia, kutoka kwa kampeni kuu za elimu kwa uanzisho mahiri za mashinani, mtindo mpya za teknolojia, mambo ya muundo msingi pia na mada zinazohusika na masomo ya maisha katika Bara.
Kujua zaidi, tafadhali tembelea www.ela-newsportal.com.
eLearning Africa, 6th International Conference on ICT for Development, Education and Training
May 25–27, 2011
Mlimani City Conference Centre, Dar es Salaam, Tanzania
Organisers: ICWE GmbH, www.icwe.net, Government of the Republic of Tanzania
Contact: ICWE GmbH, Ms Katharina Goetze,
info@elearning-africa.com, www.eLearning-africa.com
Tel.: +49 (0)30 310 18 18-0
Press Contact
ICWE GmbH
Ms Beate Timmer
Tel.: +49 (0)30 310 18 18-0, press-service@icwe.net
Press releases
www.elearning-africa.com/press_release.php
Photographs
www.elearning-africa.com/media_library_galleries.php
News Portal
www.elearning-africa.com/eLA_Newsportal
www.ela-newsportal.com